Episodes

  • Serikali imejitolea kuwalinda wakenya dhidi ya majanga asema Mwanaisha Chidzuga
    May 8 2024

    Naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga amesema serikali ya Rais William Ruto imejitolea kuhakikisha wakenya wanalindwa kutokana na majanga hasa mafuriko. Akiongea na Radio Taifa, Chidzunga amesema serikali imeweka mikakati mbali mbali kando na kuwahamisha wakenya na kuwapa makao wakenya walioathirika na mafuriko. Aidha amewasihi wakenya na mashirika mbali mbali kuungana ili kusaidia wakenya zaidi.

    Show More Show Less
    45 mins
  • Zinga: Umuhimu wa Chanjo katika afya ya mwanadamu
    Apr 26 2024

    Chanjo zimesaidia kuokoa maisha mamilioni ya watu duniani kote katika kipindi cha miaka 100 iliyopita, zimekuwa ni hakikisho kwa makuzi salama ya watoto na afya bora kwa watu wazima.

    Hata hivyo, wataalamu wamebaini hali ya ongezeko la kukataa kutumia chanjo katika baadhi ya maeneo duniani.

    Show More Show Less
    38 mins
  • Zinga: Walioidhinisha ujenzi wa nyumba kwenye njia za mito wachukuliwe hatua, asema Pius Masai Mwachi
    Apr 25 2024

    Mtaalamu wa majanga Pius Masai Mwachi ametaka serikali kuwachukulia hatua kali, maafisa wa umma ambao waliidhinisha ujenzi wa majengo/nyumba kwenye njia za mito ambazo zimesombwa na kusababisha vifo kutokana na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa humu nchini wakati huu.

    Show More Show Less
    33 mins
  • Zinga: Mwelekeo wa Siasa za chama cha ANC ni Upi ?
    Apr 24 2024

    Licha ya siasa za muungano wa Kenya Kwanza kwamba vyama tanzu vya muungano huo vivunjiliwe mbali, mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha ANC Kelvin Lunani anasema chama hicho kiko imara na kina mipangilio yake ya siasa, je kitavunjiliwa mbali ?

    Show More Show Less
    49 mins
  • Zinga: Viwango vya mafunzo ya udereva nchini viko chini, Alfayo Otuke
    Apr 23 2024

    Kulingana na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani Alfayo Otuke, Asilimia 30 ya madereva wako na leseni bandia za kuendesha gari, na kwamba Viwango vya mafunzo ya udereva nchini viko chini.

    Show More Show Less
    51 mins
  • Zinga: Wengi wa waathiriwa wa machafuko ya baada ya Uchaguzi wa 2007 wanahangaika
    Apr 12 2024

    Kulingana na Leah Aoko kutoka shirika la Utu Wetu ambalo linafanya kazi la kuwashughulikia wahanga wa machafuko ya baada uchaguzi , waathiriwa wengi wanaishi na hofu ya maisha na machungu ya kuwapoteza wapendwa wao, baadhi yao wakingojea kufidiwa.

    Show More Show Less
    50 mins
  • Zinga: Wauguzi hawajagoma, mkuu wa wauguzi Nairobi atoa hakikisho
    Apr 11 2024

    Mkuu wa wauguzi hapa jijini Nairobi amepuuzilia mbali taarifa kwamba wauguzi wangeungana na madaktari katika kuishinikiza serikali kutimiza matakwa yao. Boaz Onchari amesema hakuna sheria inayosema waungane na madaktari wanapogoma huku akishtumu wanaompiga vita katibu mkuu wa wauguzi Seth Panyako.

    Show More Show Less
    45 mins
  • Zinga: Kuwasherehekea na kuwatambua mashujaa wa Imani
    Apr 10 2024

    Wakfu wa Heroes and Heroines unatazamia kuwasherehekea wakristu na waumini waliohudumu kwa muda mrefu na ambao kujitolea kwao katika safari ya mahubiri kumegusa maisha ya watu wengi.

    Show More Show Less
    34 mins