Meza Huru cover art

Meza Huru

Meza Huru

Written by: Meza Huru
Listen for free

About this listen

Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.Meza Huru Music
Episodes
  • Mezani na ASHA BARAKA #24
    Feb 14 2025

    AshaBaraka ni nani? Asha Baraka ni ASHA BARAKA. Unaweza kwenda mbali zaidi ukamuitaMama wa muziki wa dansi Tanzania na usiwe umemzidishia sifa. Asha Barakamwanamichezo kutoka Tabora Girls, Bima hadi kua kocha wa Netball(mpira wapete).

    Lakinileo tunakubaribisha kwenye safari yake kama mwanamke wa kwanza kumiliki bendiya muziki wa dansi Tanzania na mtanzania pekee ambae anaweza sema asilimiakubwa ya wanamuziki wanaofanya mziki wa dansi leo hii wamepita chini ya uongoziwake, iwe ni bendi au chuo cha kufundishia muziki.

    Jeni nani walikua wasanii wa kwanza kabisa Twanga? Banza Stone alikua mahirikiasi gani? Unafahamu Luiza Mbutu alifika fikaje Twanga? Kwanini Ally Chokianaitwa kinanda?

    Yotehaya ameyanyoosha kuweka rekodi sawa. Na ziada si haba. Karibu mezaniumsikilize The Ironylady, Mama, Bibi, Mkurugenzi na Chairman ila sisi tunamuitaNguzo kubwa ya mziki wa dansi Tanzania.

    Show More Show Less
    1 hr and 29 mins
  • Mezani na TAJI "MASTER T" LIUNDI #23
    Jan 3 2025

    Kama ulishawahi kuisikia ile story ya mtangazaji wa kwanza kucheza wimbo wa Bongo Fleva kwenye radio. Mtangazaji huyo, leo amepata nafasi ya kutubariki na historia yake. Jinsi alivyochangia muziki huu kuwa kimbilio la vijana wengi sana kama sehemu ya ajira yao.


    Jina lake kamili ni Taji George Liundi au MASTER T kama alivyobatizwa na Charles Hillary. Kuanzia alivyoanza kutangaza Redio One, moja ya vipindi vyake vya awali kabisa cha DJ Show, kabla ya kuwaachia mikoba wakina Mike Mhagama baada ya kuikacha Redio one na kwenda kufanya kazi kwenye media zingine.


    Karibu mezani umfahamu zaidi.

    Show More Show Less
    4 hrs and 13 mins
  • Mezani na LUCCI #22
    Nov 1 2024

    Marehemu CPWAA anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (KING OF BONGO FLEVA CRANK) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na LUCCI chini ya Mawingu Studio. Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank. Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.

    Show More Show Less
    1 hr and 54 mins
No reviews yet