TANAPA PODCAST cover art

TANAPA PODCAST

TANAPA PODCAST

Written by: Tanzania National Parks (TANAPA)
Listen for free

Welcome to the official podcast of the Tanzania National Parks (TANAPA). Join us as we explore key conversations on conservation education, tourism, and investment opportunities across Tanzania’s National Parks. Each episode highlights strategies for sustainable conservation and the vital partnerships that help protect our natural resources for current and future generations.Tanzania National Parks (TANAPA) Political Science Politics & Government
Episodes
  • TANAPA PODCAST EPISODE 16: MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI.
    Nov 24 2025

    Episodi hii inaangazia njia za asili zilizotumika katika utunzaji wa maliasili kwa kufuata taratibu za kitamaduni, mila, desturi na makatazo mbalimbali yaliyosaidia kusimika mizizi imara na kuwa chimbuko la uhifadhi wa kisasa. Hekima za mababu zetu kama vile kuheshimu misitu, kutotumia rasilimali kupita kiasi, na kutambua uhusiano wa binadamu na mazingira vimekuwa dira muhimu inayoongoza mbinu za kisayansi za leo kwenye uhifadhi endelevu.


    Sikiliza simulizi hii ya kuvutia katika Epsodi ya 16.


    Mwongoza kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena.


    Mgeni I: Mzee Rashid Shabani

    Kitopeni.

    Mgeni II: Mzee Ramadhani Nyundo

    Usikose kila Jumatatu kupitia Platform za TANAPA Podcast.


    TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

    Show More Show Less
    36 mins
  • TANAPA PODCAST EPISODE 15: UHIFADHI NI JUKUMU LA KILA MMOJA
    Nov 17 2025

    Episodi hii inakuletea uchambuzi wa kina kuhusu Uhifadhi kwa kuzingatia kuwa Uhifadhi wa wanyamapori ni zoezi la kujitolea kulinda na kuhifadhi maliasili kwa maslahi ya Taifa kwa kizazi hiki ma kijacho.


    Sikiliza Episodi ya 15 upate elimu kutoka kwa Mzee Ibrahimu Kasontola kutoka katika kijiji cha Lukoma wilayani Uvinza - Kigoma aliyejitolea kwa hali na mali kuhifadhi msitu katika eneo la makazi yake na kupelekea eneo hilo kuwa makazi ya kudumu ya Sokwemtu sanjari na kupanda migomba ambayo hutumika kama chakula pendwa cha wanyamapori hao ambao mara nyingi utawakuta katika makazi ya mzee huyo.


    Mwongoza Kipindi: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena.


    Wageni

    1.⁠ ⁠Ibrahim Kasontola (Mzee anayewahifadhi Sokwemtu hao).

    2.⁠ ⁠Mwatano Omary (Mke wa Mzee Ibrahim Kasontola).

    3.⁠ ⁠⁠Afisa Uhifadhi Mwandamizi - Lameck Matungwa Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Milima Mahale

    Usikose kila Jumatatu kupitia Platform za TANAPA Podcast.

    TANAPA PODCAST, HIFADHI ZETU, SAUTI YETU.

    Show More Show Less
    1 hr and 3 mins
  • TANAPA PODCAST EPISODE 14: MILA, DESTURI NA TAMADUNI KATIKA UHIFADHI WA MALIASILI.
    Oct 27 2025

    Episodi hii inaangazia mila, desturi na tamaduni katika uhifadhi wa maliasili, hususan namna jamii ya Wangoni kutoka mkoani Ruvuma ilivyotumia majina na utamaduni wao kulinda Wanyamapori na Misitu tangu enzi za mababu zetu.

    Hadithi hii ya kuvutia inaonesha jinsi urithi wa jadi ulivyokuwa chachu ya kulinda rasilimali za Taifa ambazo leo hii zinachangia kwa kiasi kikubwa katika sekta ya uhifadhi na utalii.

    Sikiliza simulizi hii adhimu kutoka kwa Chifu Songea Mbano wa Kwanza, kupitia TANAPA Podcast – Episode ya 14.


    Mwongozaji: Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Catherine Mbena
    Mgeni: Samweli Vitus Mbano (Chifu Songea Mbano I)


    Usikose kila Jumatatu na Alhamisi kupitia majukwaa mbalimbali ya TANAPA Podcast

    Show More Show Less
    55 mins
adbl_web_anon_alc_button_suppression_t1
No reviews yet