Episodes

  • AI na Ubunifu wa Injili | Je, AI Inaua Creativity au Inaiinua? | Ft. Innocent Mwagilo
    Jun 27 2026

    Send us Fan Mail

    Katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wetu kuhusu AI na Ubunifu wa Injili, tunazungumza na Innocent Mwagilo — Music Producer, Songwriter na Sound Engineer.

    Katika mazungumzo haya tunachunguza namna Artificial Intelligence (AI) inavyoendelea kubadilisha music production na ubunifu kwa ujumla. Je, AI ni tool nyingine tu kama tulivyozoea kutumia studio software, au imeanza kuchukua nafasi ya creativity ya mwanadamu?

    Hili si mjadala wa kupinga au kuunga mkono AI.

    Ni mazungumzo ya kutafuta hekima, kuelewa mabadiliko yanayotokea, na kujiuliza jinsi Wakristo wanavyoweza kuitumia teknolojia kwa namna inayomheshimu Mungu.

    🎙️ Guest: Innocent Mwagilo
    Music Producer | Songwriter | Sound Engineer

    Karibu Tikvah Podcast.

    Show More Show Less
    42 mins
  • Yusufu: Kivuli cha Kristo
    Jun 21 2026

    Send us Fan Mail

    Simulizi la Yusufu siyo tu hadithi ya kutoka gerezani kwenda ikulu. Ni picha inayotuelekeza kwa Kristo.

    Yusufu alikuwa mwana aliyependwa na baba yake, akakataliwa na ndugu zake, akauzwa kwa fedha, akateseka bila hatia, na hatimaye akainuliwa ili kuhifadhi uhai wa wengi.

    Kwa namna kubwa zaidi, yote haya yanatuelekeza kwa Yesu Kristo — Mwana mpendwa wa Baba, aliyekataliwa, aliyeteseka, na kupitia mateso yake akaleta wokovu kwa ulimwengu.

    Katika kipindi hiki tunatafakari kwa nini Misri haikuwa nyumbani kwa Yusufu, na kwa nini Mkristo hapaswi kujenga tumaini lake juu ya mafanikio, mamlaka, mali, au nafasi aliyonayo, bali juu ya Kristo na uzima wa milele.

    Karibu kusikiliza Tikvah Podcast.

    Show More Show Less
    45 mins
  • Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?-Episode 3
    Jun 8 2026

    Send us Fan Mail

    Katika Episode hii nimefanya mazungmzo na kaka yangu na mwalimu wangu Faith Joel Shimba Kuhusu namna kanisa limejikuta likibobea katika shughuli za kiroho na kusaua kuhusu Mungu

    Show More Show Less
    57 mins
  • Uchambuzi wa Nyimbo-Kitabu by Paul Clement
    May 27 2026

    Send us Fan Mail

    Tumejadili kuhusu live record ya wimbo wa Paul Clement Kitabu(Ajabu) wimbo unapatikana kwenye Youtube channel yake Paul Clement pamoja na Digital Platform zote, tumejadili kuhusu ubora wa utunzi ubora na ubora wa video

    Karibu kusikiliza

    Show More Show Less
    20 mins
  • Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?-Episode 2
    May 27 2026

    Send us Fan Mail

    Katika episode hii tunachunguza namna ambavyo baadhi ya huduma na makanisa ya kizazi hiki yamehamisha watu kutoka kumtafuta Kristo kwenda kushikilia mbinu, ishara, na experiences za kiroho.

    Kutoka matumizi ya mafuta, maji, udongo, vitambaa, prophetic acts, hadi “gymnastics” nyingi za kiroho , tunajiuliza: Je, hizi ni njia zinazotupeleka kwa Mungu, au zimekuwa distraction inayochukua nafasi ya ujumbe wa kweli wa Injili?

    Kupitia mifano ya Yesu Kristo na mitume:

    • Yesu kutumia mate na udongo kumponya kipofu,
    • Kulisha watu 5000 kwa mikate na samaki,
    • Petro kuponya kupitia kivuli chake,
    • Paulo kupitia leso na vitambaa,

    tunagundua jambo moja muhimu:

    Walifanya miujiza, lakini hawakuwahi kujenga huduma zao juu ya miujiza.

    Ujumbe wao ulikuwa mmoja:
    Kuwaleta watu kwa Mungu.

    🎙 Episode hii ni mwaliko wa kurudi kwenye Injili halisi, kumtafuta Kristo kuliko ishara, na kuhakikisha hatupendi “mkate” kuliko “Bread of Life”.

    #ChristianPodcast #SwahiliPodcast #Injili #Faith #JesusChrist #ChristianLife #Truth #RelationshipWithGod

    Show More Show Less
    11 mins
  • Imani Kwa Mungu Au Imani Kwa Mbinu?
    May 21 2026

    Send us Fan Mail

    Katika episode hii tunazungumzia tofauti kati ya kumwamini Mungu na kuamini mbinu za kiroho. Mara nyingi waamini tunajikuta tukiegemea sana maombi, kufunga, ibada, na taratibu mbalimbali za kiroho kiasi kwamba tunasahau kuwa vitu hivi vilikusudiwa kutupeleka kwa Mungu — sio kuchukua nafasi ya Mungu mwenyewe.

    Kupitia simulizi la Musa na mwamba, pamoja na mafundisho ya Yesu kuhusu mapokeo, tunatafakari namna ambavyo mbinu zinaweza kuwa muhimu kuliko uhusiano wa kweli na Mungu.

    Je, bado tunamtafuta Mungu… au tumebaki kushikilia mifumo?

    🎙 Mada hii ni mwaliko wa kurudi kwenye imani ya kweli, ushirika wa kweli, na kumtumaini Mungu zaidi ya tulivyozoea kufanya mambo ya kiroho.

    #Faith #ChristianPodcast #Imani #RelationshipWithGod #ChristianLife #Jesus #SwahiliPodcast

    Show More Show Less
    11 mins