• EP10 TENOVERTEN- Mafanikio ya Kiroho na Kiakili- Authentic Swahilians
    Dec 23 2024

    Episode 10: Mafanikio ya Kiroho na Kiakili: Je, Maendeleo ni ya Kiuchumi Pekee?

    Katika kipindi hiki cha TEN OVER TEN Podcast, tunazama katika mjadala wa kipekee unaozungumzia mafanikio yanayozidi mipaka ya kiuchumi. Je, kweli maendeleo yanapimwa tu kwa pesa na mali? Jackson na mgeni wake Kefa Victor wanajadili umuhimu wa mafanikio ya kiroho na kiakili kwa maisha yenye utulivu na maana.

    Kwa Nini Usikilize?

    • Sehemu ya Kwanza: Fahamu jinsi utulivu wa kiroho unavyochangia afya ya kiakili na hata kusaidia kufanya maamuzi bora ya kifedha.
    • Sehemu ya Pili: Pata mbinu za kujenga mafanikio ya kiakili kupitia kutafakari, kujisomea, na kujizunguka na watu wenye maono chanya.
    • Sehemu ya Tatu: Tambua mtazamo wa jamii kuhusu mafanikio ya kiroho na umuhimu wa kuwa na mshauri wa kiroho.

    Nini Unapaswa Kujifunza?

    • Jinsi ya kuleta uwiano kati ya maendeleo ya kiroho, kiakili, na kiuchumi.
    • Namna ya kuwekeza katika afya yako ya kiakili na kuimarisha maono yako ya maisha.
    • Umuhimu wa kuishi maisha yenye maana, zaidi ya mbio za kila siku za kiuchumi.

    Jiunge nasi na ugundue siri za mafanikio ya kweli! 🌟

    Show More Show Less
    1 hr and 7 mins
  • EP09 TENOVERTEN- Kujenga Nidhamu na Maadili Imara: Msingi wa Ukuaji- Authentic Swahilians
    Dec 16 2024

    Katika episode hii ya 9 Jackson na Kefa wanachambua umuhimu wa nidhamu, wakitumia mifano halisi kama Cristiano Ronaldo, ambaye nidhamu yake ya hali ya juu kwenye mazoezi na maisha ilimfikisha kilele cha mafanikio ya kimataifa. Wanashiriki pia mbinu madhubuti za kujenga nidhamu, kama kuweka malengo wazi, kujifunza kusema hapana kwa vishawishi, na kufuatilia maendeleo yako kwa ukaribu.

    Mambo Muhimu Utakayojifunza:

    • Nidhamu ni injini ya maisha na ufunguo wa kufanikisha ndoto zako.
    • Maadili hufanikisha uaminifu, ambao ni muhimu kwa mafanikio ya kudumu.
    • Mbinu za vitendo za kujenga nidhamu na kudumisha maadili katika mazingira magumu.
    Show More Show Less
    1 hr
  • EP08 TENOVERTEN-"Rafiki au Adui? Watu Wanaokuzunguka na Ukuaji Wako"-Authentic Swahilians
    Dec 9 2024

    Katika episode hii ya 08 Jackson na Kefa Victor wanazungumzia jukumu muhimu la watu wanaokuzunguka katika safari yako ya mafanikio. Wanajadili jinsi ya kuchagua marafiki kwa busara ili kukuza uhusiano wenye afya na unaosaidia ukuaji wako wa binafsi na kitaaluma.

    Show More Show Less
    1 hr and 13 mins
  • EP07 TENOVERTEN-Ubunifu na Kujiajiri: Fursa za Ukuaji Katika Ulimwengu wa Kisasa-Authentic Swahilians
    Dec 2 2024

    Katika episode hii ya saba cha TEN OVER TEN Podcast, tunazungumzia mada ya kuchochea fikra na vitendo: Ubunifu na Kujiajiri. Katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi, ubunifu ni silaha ya kufanikisha ndoto na kutengeneza nafasi mpya za ajira. Tukiongozwa na Jackson na Kefa Victor, Pamoja na mgeni Mr Saad tunachambua kwa kina:


    • Umuhimu wa ubunifu katika soko la kisasa la kazi na biashara.
    • Fursa zilizopo kwa wale wanaotaka kujiajiri na jinsi ya kuzitumia.
    • Changamoto zinazowakumba vijana na mbinu za kuzikabili.
    • Jinsi teknolojia inavyoweza kuwa chombo kikuu cha ubunifu na ajira.
    • Njia za kukuza biashara za kibunifu na nafasi ya serikali katika kusaidia wabunifu.
    Show More Show Less
    1 hr and 41 mins
  • EP06 TENOVERTEN-Kujifunza Kutoka kwa Changamoto: Kutokata Tamaa- Authentic Swahilians
    Nov 25 2024

    Katika episode hii ya sita, Jackson na Kefa wanajadili umuhimu wa changamoto katika maisha na jinsi ya kuzigeuza kuwa fursa za ukuaji. Wanatoa mifano hai, kama safari za Nelson Mandela, J.K. Rowling, na Elon Musk, zikionyesha jinsi changamoto zinavyoweza kukuimarisha kiakili, kimaadili, na hata kufanikisha ndoto zako. Kwa mazungumzo yenye maarifa na hamasa, utajifunza mbinu za kushinda changamoto kwa ubunifu, kuendelea mbele, na kutumia uzoefu wako kuhamasisha wengine.

    Show More Show Less
    1 hr and 3 mins
  • EP05 TENOVERTEN -Kubadilisha Makazi au Nchi – Je, Kunaweza Kuleta Maendeleo Binafsi?- Authentic Swahilians
    Nov 18 2024

    Katika episode hii ya 5 tunajadili mada inayogusa maisha ya wengi: Kubadilisha Makazi au Nchi – Je, Kunaweza Kuleta Maendeleo Binafsi? Jackson Lusagalika na Kefa Victor wanaangazia faida, changamoto, na mbinu za kufanikiwa unapochukua hatua ya kuhamia nchi au makazi mapya.


    Tutashuhudia mifano hai ya watu maarufu kama Elon Musk, Lupita Nyong’o, na Chimamanda Ngozi Adichie, ambao walifanikiwa kutumia fursa za kubadilisha nchi kuendeleza ndoto zao. Pia, changamoto kama utambulisho wa kitamaduni, umbali na familia, na changamoto za kisheria zinajadiliwa kwa kina.

    Show More Show Less
    58 mins
  • EP04 TENOVERTEN-Mahusiano ya Mapenzi na Maendeleo ya Kibinafsi-Authentic Swahilians
    Nov 11 2024

    Katika episode hii, Jackson na Kefa wanazungumzia jinsi mahusiano ya mapenzi yanavyoweza kuchangia ama kudhoofisha maendeleo binafsi. Wanachambua faida za kuwa na mahusiano yenye afya kama msaada wa kisaikolojia na utulivu, huku wakionya juu ya athari za mahusiano yenye migogoro kwa malengo na nidhamu binafsi. Pia wanajadili umuhimu wa kuweka uwiano kati ya mapenzi na malengo ya kibinafsi na kujua wakati wa kuachana na mahusiano yenye sumu ili kuweka mbele afya ya kiakili na mafanikio binafsi

    Show More Show Less
    1 hr and 5 mins
  • EP03 TENOVERTEN-Kufanikisha Mafanikio: Tofauti ya Mafanikio Kati ya Mtu na Mtu-Authentic Swahilians
    Nov 4 2024

    Katika Episode hii ya tatu TEN OVER TEN Podcast, tunachambua mada ya "Kufanikisha Mafanikio" na tofauti zake kati ya watu. Tunaanza kwa kuuliza, mafanikio yanamaanisha nini kwako binafsi? Na ni vigezo gani hutumika kuamua kama mtu amefanikiwa? Tunalenga kuelewa kama juhudi binafsi zinatosha au msaada wa watu wengine pia ni muhimu katika safari ya mafanikio.


    Tunaangazia zaidi tofauti za mafanikio kati ya mtu mmoja na mwingine, na iwapo mali na pesa ndizo kigezo pekee cha mafanikio. Pia tunagusia dhana za mafanikio ya kiroho na kiakili, na jinsi furaha ya ndani inavyoweza kuwa kipimo muhimu zaidi kuliko mafanikio ya kiuchumi pekee. Tunajadili jinsi mafanikio yanavyoweza kuathiri furaha ya mtu na kipaumbele cha mtu binafsi kati ya mafanikio ya kiuchumi na furaha.


    Kipindi hiki kina lengo la kutoa mwanga juu ya tafsiri tofauti za mafanikio na umuhimu wa kuzingatia hali yako ya kiuchumi, kielimu, na kijamii. Jiunge nasi katika safari hii ya kutafakari maana ya kweli ya mafanikio na kujifunza mbinu za kufanikisha ndoto zako!

    Show More Show Less
    47 mins